ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja
ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi.
Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea.
Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine.
“Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele” alisema Masoud.
Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake.
Awali abiria walisema kuwa katika hekaheka na upepo mkali meli ilipoteza muelekeo na kuelekea upande wa Tanga, kabla ya mafundi kufanikiwa kutengeneza.
Safari ya meli hiyo ilianza baada ya matengenezo yalichukua muda wa zaidi ya masaa mawili majini na kutarajiwa kufika bandari ya zanzibar ambapo ilitarajiwa ifike saa 10 jioni.
Hadi tunakwenda mitamboni meli hiyo haijafika zanzibar. Na hakuna taarifa zozote kutoka mamlaka zinazohusika kuhusiana na suala hilo licha ya wananchi kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka hizo. wakizungumza na gazeti hili wananchi mbali mbali wamesema bado serikali haijapata funzo kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali mbaya iloiyotokea mwaka jana ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
wamesema ni jambo la kushangaza kwa serikali iliyo makini kushindwa kutafuta usafiri wa uhakika na badala yake kuwaacha wananchi wake wakitumia usafiri usio na uhakika jambo ambalo wananchi wengi wanasafiria boti hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda ndege.
“Ingekuwa tuna ndege basi tungekuwa tunasafiri kwa ndege maana usafiri wa baharini imeshakuwa ni kifo sasa lakini kwa kuwa sisi ni masikini hatuna budi kucheza bahati nasimu na maisha yetu kwa sababu ndio usafiri wa watu wanyonge tutafanya nini? alihoji Haji Hamadi Mkaazi wa Mwembetanga Unguja.
Hii ni mara ya nne katiak kipindi cha wiki moja kutokea misukosuko kama hiyo inayohusu meli hiyo hiyo ya Seagul na Sea Express ambapo wananchi wamekuwa na khofu ya usafiri wa Unguja na Pemba kutokana na meli nyingi zinzofanya safari za visiwa hivyo kutokuwa na uhakika wa usalama majini.
0 comments:
Post a Comment