Thursday, May 10, 2012

Mkutano wa viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wa Kimataifa wameanza mkutano mjini Addis Ababa,Ethiopia kujadili jinsi ya kukuza maendeleo na kuvutia uwekezaji katika bara hilo.
Uchumi kuimarika
Uchumi kuimarika Afrika
Mkutano huo wa siku tatu juu ya Uchumi Duniani utaangazia masuala kama ajira, utawala bora na kutunza mazingira.
Watayarishi wa mkutano huu wanasema kua Afrika, ni bara lenye nchi sita zenye Uchumi unaokua kwa kasi Duniani na sasa bara hilo liko kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa ya uchumi.
Nigeria ni mojapo ya nchi hizo zenye Uchumi unaokua kwa kasi, lakini kama anavyoarifu mwandishi wa BBC Chris Ewokor kutoka Abuja, siyo kila mwananchi aliyenufaika na wimbi hili la mapato.
Ewokor anasema kua majuma matatu yaliyopita Waziri mdogo wa Nigeria katika Wizara ya fedha, Dr Yerima Ngama,alitangaza kua nchi hiyo ni ya tatu kwa nchi zenye Uchumi unaokua kwa haraka.
Alidokezea kua uchumi umeimarika zaidi katika sekta isiyokua ya mafuta, na kwamba serikali ilikua katika jitihada za kuuimarisha zaidi uchumi wake.
Hata hivyo matamshi ya Waziri huyo yanatokea wakati wataalamu wa masuala ya Uchumi nchini Nigeria wakieleza kua nchi hio ina idadi kubwa ya raia wanaoishi maisha duni ya ufukara.
Uchumi kwa kiwango kikubwa bado unategemea mafuta. Lakini wa Nigeria wengi ni masikini licha ya utajiri wa mafuta.
Wengi wanaishi kwa dola moja
kuishi kwa dola kwa siku
Taarifa ya Benki ya Dunia inasema kua nusu ya watu wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa kila siku.
Raia hawa wa mjini Abuja walimueleza mwandishi wetu hisia zao kuhusu kukua kwa uchumi.
1 ("Nina amini kua nimejitahidi kwa kila njia na nilicho nacho nimekitumikia. Sidhani kama nimehisi lolote kutokana na hali hio ya uchumi. Nchi hii ni tajiri kutokana na mali asili tuliobarikiwa nayo.''
2 ("Kwangu mimi, sioni lolote litakalonifaa. Hii ni kwa sababu tangu mwaka 2003 niliacha masomo, na kuingia mitaa kuhangaika kutafuta maisha. Kodi ya nyumba ni shida hivo nitasemaje kua uchumi ni mzuri. Sijahisi lolote kuhusu uchumi.''
3 ("Uchumi huu hauwezi kutupendelea sababu hatuelewi wanachoufanyia Uchumi. Sisi raia masikini walio wengi, sidhani hata kama wanaweza hata kutufikiria sisi, mawazo yao yanaelekea kupakia mapesa kwa manufaa yao kwanza na watoto wao.
Ni Mngu atakayewapokonya utajiri kutoka mikononi mwaka.")
Ukosefu wa ajira na ufukara yamechangia kuchochea uhalifu na ukosefu wa usalama, pia tatizo la umeme line maana kwamba viwqanda vya humu nchini vimeathirika mno kwa sababu havina uwezo wa kumudu majenereta.
Watu wengi wanalaumu rushwa miongoni mwa maofisa wa serikali kua kitovu cha kubomoka kwa miundo mbinu.
Baadhi ya wataalamu wameonyesha imani kua ingekua bora uchumi mzuri ungekua bora kama ungeondoa shida ya kukosa ajira na kupungua kwa umasikini.
Huduma za umma, ubora wa maisha na kuishi maisha marefu ndio chachu ya Uchumi mzuri.
Wakati huu ambapo Uchumi unaonekana kumilikiwa na wachache, raia waliobaki wanaishi kwa umasikini wa kupindukia.

0 comments:

Post a Comment