- Magazeti
ya udaku likiwemo hili la Globe yamekuwa yakiandika, tena kama habari
kuu katika ukurasa wa mbele kabisa, kwamba Obama ni/alikuwa shoga.
Mwanaume mmoja aitwaye Larry Sinclair amekuwa akidai kwamba alikuwa
mpenzi wa Obama kwa miaka mingi wakati ule akiwa bado seneta kule jimbo
la Illinois; na kwamba walikuwa wanatumia madawa ya kulevya pamoja.
Kashfa hizi zilianza zamani wakati Obama bado akiwa mgombea wa uraisi na
bado zinaendelea. Larry Sinclair amekuwa akidai kwamba yeye pamoja na
mwanaume mwingine shoga aliyekuwa mwimbishaji wa kwaya katika kanisa la
zamani la Obama kule Chicago (huyu aliuawa mwaka 2007) waliwahi kuwa na
uhusiano wa kishoga na Obama. Hata hivyo alipopewa "polygraph test" ili
kuweza kujua kama alikuwa anasema ukweli ama la kuhusu kashfa hizi,
alishindwa na matokeo yalionyesha kwamba alikuwa anadanganya.
- Nyumbani
sisi bado tunafikiri kwamba kila kitu kinachoandikwa katika gazeti au
kuwekwa mtandaoni ni cha kweli lakini hawa wenzetu wanajua kwamba huu ni
udaku na hakuna mtu ambaye anajali. Ndiyo maana Obama aliweza kushinda
uraisi pamoja na magazeti haya kuandika udaku wote huu. Siku
tutakapoweza kung'amua kwamba mambo mengi yanayosemwa katika magazeti
(hasa haya ya udaku yaliyofumuka kila kona ili kuishibisha kiu ya
utandawazi) ama si ya kweli au hayajathibitishwa basi tutakuwa tumepiga
hatua kubwa. Nimeandika makala ndefu yenye kichwa "Ze Utamu Imetufundisha Nini?" kuhusu jambo hili na makala hiyo itatoka katika gazeti la Kwanza Jamii la Jumanne tarehe 16/6/2009. Nitaiweka hapa baadaye kidogo.
CHANZO CHA HABARI: http://matondo.blogspot.com/2009/06/magazeti-ya-udaku-obama-ni-shoga.html
0 comments:
Post a Comment