Jopo la wataalamu wa masuala ya
afya nchini Marekani kwa mara ya kwanza limeafiki na kuunga mkono dawa
ambayo inaweza kutumika kama kinga dhidi ya virusi vinavyoeneza ukimwi.
Jopo hilo limependekeza kwa Mamlaka inayosimamia
chakula na Dawa nchini Marekani dawa wakubali dawa aina ya
Truvada,itumiwe na watu ambao wamo hatarini kukumbwa na virusi
vinavyosambaza ukimwi.
Hata hivyo Jopo hilo halina mamlaka juu ya wakuu hao ingawa mara nyingi hukubaliana.
Wahudumu kadhaa wa Afya pamoja na makundi yanayoshughulikia tatizo la ukimwi wamepinga dawa hio isiruhusiwe.
Hata hivyo, wandishi wanasema kua hatua hio inaweza kutokea kua muhimu katika vita dhidi ya ukimwi.
Tayari dawa ya Truvada imeisha idhinishwa na
mamlaka hio ya dawa na chakula kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi,
ikitumiwa sambamba na dawa zilizopo maarufu kama ''anti-retroviral
drugs''.
Utafiti uliofanywa mnamo mwaka 2010 ulionyesha
kua 'Truvada', iliyotengenezwa na kampuni yenye makao yake huko
Carlifornia, Gilead Sciences, kwa kiwango ilipunguza hatari ya
kuambukizwa ukimwi miongoni mwa wanaume wenye tabia ya kufanya mapenzi
na wanaume wenzao kwa asili mia 44% na 73%.
Uwamuzi mwezi Juni
Kamati inayotoa ushauri kuhusu dawa
zinazostahili kutumiwa kwa kukabiliana na ukimwi, FDA, ilipitisha kwa
kura 19 kwa 3 kuafiki dawa hii itumiwe na watu ambao wamo katika hatari
kubwa kuweza kuambukizwa - wanaume ambao wana tabia ya uzinzi na wanaume
wenzao wengi.
Vilevile waliidhinisha dawa hii kwa kura nyingi,
itumiwe na watu ambao hawajaambukizwa lakini wakiishi na wapenzi ambao
tayari wanaishi na virusi vya ukimwi na halikadhalika kwa makundi
yanayotazamiwa kua hatarini kuambukizwa ukimwi kupitia shughuli za
ngono.
Upinzani kwa dawa hii ulitegemea dhana kua
inaweza kutoa sura kwa mtumiaji kujihisi kua ana kinga mwilini, na hivyo
kutoka ovyo, na pili hofu ya dawa hii ni uwezekano wa kuzua balaa la
ukimwi mpya usiokubali dawa au tiba.
Vilevile kuna wasiwasi kua bei kali ya Truvada
inaweza kuathiri kiwango cha fedha za shughuli nyingine za kutafuta dawa
yenye bei nafuu kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Muuguzi mmoja Karen Haughey aliliambia Jopo kua :
"dawa hii 'truvada' lazima itumiwe kila siku, wakati wote, siku hadi
siku, asili mia 100% ya mda wako, na kwa uzowefu wangu naona kama hilo
halitowezekana.
Hata hivyo wauguzi wengi walifurahia pendekezo la Jopo.
Mkurugenzi mtendaji wa juhudi za kinga ya virusi
vya ukimwi, Mitchell Warren alisema baada ya kura hio kua "hili
linatufikisha ukingoni mwa kufanikiwa katika kupata kinga dhidi ya
ukimwi.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) inatarajiwa kufikia uwamuzi wake kabla ya tareh 15 Juni.V
0 comments:
Post a Comment