WANAFUNZI 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaokabiliwa na
kesi ya kufanya mkusanyiko haramu, wamesomewa maelezo ya awali katika
kesi yao hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam.
Aidha Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Waliarwande Lema amepanga kesi hiyo ianze kusikilizwa Juni 25 na 26 mwaka huu.
Katika maelezo hayo yaliyosomwa jana na Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi, Lema walidaiwa kuwa pamoja na kupewa ishara ya kusitisha maandamano na askari wa Jeshi la Polisi walikiuka na kuwashambulia askari kwa mawe.
Komanya alidai kuwa Novemba 11, 2011 wanafunzi hao walifanya mkusanyiko katika Uwanja wa Revolution lililopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye waliandamana kuelekea eneo la Ubungo Maji huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaoilaumu Serikali na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuwa haiwatendei haki.
Ilidaiwa wanafunzi hao walifika Ubungo maji ambapo walikutana na askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) ambao walitoa tamko na ishara zaidi ya mara tatu kuwataka kusitisha maandamano hayo na wasambae kurudi walipotoka lakini walipinga amri hiyo.
Askari walianza kuwakamata wanafunzi hao na kuwafikisha katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo Mei 14,2011 walifikishwa mahakamani.
Alidai katika muhula wa masomo wa mwaka 2011/2012 wanachuo kutoka vitivo mbalimbali walikuwa hawajapata mikopo kutokana na sababu mbalimbali na walielezwa na utawala juu ya tatizo hilo.
Wakati taratibu hizo zinafanyika ndipo kulijitokeza kikundi kilichojiita Kikosikazi ambacho kiliundwa na wanafunzi wanne ambao ni Mwambapo Elias, Evarist Ambros, Baraka Bonas na Alphonce Lusako.
Kilianza kuweka msukumo kwa uongozi wa Serikali ya Wanafunzi(Daruso) kuchukua hatua haraka bila kujali kama wanafunzi hao wana vigezo au la.
Novemba 9, 2011 kikundi hicho cha Kikosikazi kiliwashawishi wanafunzi wenzao kwa kufanya mkutano usio halali na usiotambulika kisheria ambapo waliweka mpango wa namna ya kutekeleza mgomo na wakakubaliana uwe Novemba 11, 2011 siku ambayo walitekeleza azma hiyo.
Novemba 14, mwaka huu wanafunzi hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza wakidaiwa kufanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo la UDSM.
Pia wanadaiwa kukaidi amri halali ya Polisi ya kuwataka watawanyike.

0 comments:
Post a Comment