Monday, May 21, 2012


DORIS MALIYAGA
UONGOZI wa Simba umetangaza kuwa hautaitumia tena jezi namba 30 aliyokuwa akiivaa Patrick Mafisango lakini pia rafiki kipenzi wa marehemu huyo, Haruna Moshi Boban alijikuta akikosa raha na kukimbilia chooni kutokana na kuzongwa na mashabiki wa soka.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema jana Ijumaa kuwa: "Uongozi wa Simba, umekubaliana kutoitumia jezi namba 30 iliyokuwa ikitumiwa na marehemu. Haitatumika tena, itabaki kuwa kumbukumbu."

Boban ambaye ambaye alikuwa ameondoka baada ya kuaga mwili alirudi kwa mara nyingine katika Uwanja wa Sigara, Chang'ombe alikohitajika kwa ajili ya kumsindikiza rafiki yake, Mafisango ambaye alitakiwa kuondolewa mahali hapo na kupelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhifadhiwa kwa ajili ya safari leo Jumamosi kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alipofika uwanjani hapo, Boban ambaye alikuwa rafiki wa karibu na ndiye alikuwa alilala naye chumba kimoja Mafisango wanapokuwa katika kambi ya klabu hiyo, mashabiki waliokuwa wakiaga mwili wa marehemu, mara baada ya kumwona anaingia uwanjani hapo, walifurika wote na kumfuatilia kwa nyuma ilimradi wamwone na kutuliza nafsi zao.

Baada ya Boban kuona hivyo, alikwenda moja kwa moja hadi vilipo vibanda vya kupumzikia, ulipo uwanja wa kikapu na kukaa chini, hapo akawa kama amewapa nafasi mashabiki kumzunguka wakimshangaa.

Kuona vile, Boban aliondoka na kwenda vilipo vyoo vya ndani vya ukumbi huo, baadaye alifunguliwa mlango wa ziada ulipo upande huo.

Katika mlango huo, kuna nga
zi za kupandia juu ambako ndiko alijificha na kukaa huko takribani muda wa nusu saa na alitoka ilipofika wakati safari ya kwenda Uwanja wa Ndege ambako mwili wa Mafisango ulilazwa kabla ya safari ya leo Jumamosi alfajiri.

0 comments:

Post a Comment