TAARIFA za kwamba Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imebaini
kuwa Jeshi la Polisi lina askari 700 wenye majina yanayofanana na
waajiriwa wengine serikalini huku Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
likiwa na askari 248 zimeshtua taifa.
Taarifa hizi za kutisha
zilipatikana baada ya Nida kuanza utekelezaji wa kuwapatia wafanyakazi
wa Serikali vitambulisho vya taifa katika Jiji la Dar es Salaam kabla ya
kuwapatia watu wa kada nyingine nchini kote.
Kutokana na uchambuzi wa Nida, polisi na wanajeshi hao wamebainika kutumia cheti kimoja na wafanyakazi wengine wa Serikali kitendo ambacho ni kosa la kisheria.
Kutokana na uchambuzi wa Nida, polisi na wanajeshi hao wamebainika kutumia cheti kimoja na wafanyakazi wengine wa Serikali kitendo ambacho ni kosa la kisheria.
Kutokana
na jambo lenyewe kuwa nyeti na ambalo litakiwa kufanyiwa ufuatiliaji wa
haraka, tayari Jeshi la Polisi limeunda tume ya kuchunguza kashfa hii
ya vyeti ndani ya taasisi yake.
Hakika ni jambo lisiloweza
kufikirika kwamba taasisi zetu muhimu za kulinda raia na mali zao,
kulinda mipaka yetu zina wafanyakazi ambao hawana maadili kiasi cha
kuthubutu kughusi vyeti kwa lengo la kupata ajira.
Tunaamini
kwamba watumishi wa aina hii si hatari ndani ya jeshi, lakini ni hatari
kwa raia kwani wanaweza kufanya lolote hata kama linakiuka maadili ya
kazi zao kwa kuwa wao wameweka maslahi binafsi mbele, uadilifu wa kazi
wameuweka kando.
Ndio maana leo katika majeshi yetuna idara kadhaa
za Serikali kuna watumishi wengi wasio na maadili kazini kwa kuwa
hawajasomea fani husika, bali wametumia njia za hila kupata ajira hizo
kama Nida walivyobaini.
Ndio maana tunawapongeza Nida kwa kuweza
kugundua kashfa ambayo huenda ikawakumba wengi zaidi hasa pale ambapo
wataanza kutoa vitambulisho nchi nzima na hasa kwenye Halmashauri za
Wilaya ambako tunaambiwa kuwa kuna idadi isiyo na kifani ya watu
wanaotumia vyeti vya watu wengine, wakiwamo walio hai na waliokufa.
Idadio
hii kubwa ya waajiriwa wa Serikali wamefanya udanganyifu mkubwa na
wanachostahili baada ya uchunguzi kukamilika ni kufukuzwa kazi na
kufunguliwa kesi za jinai kwa kughushi ili iwe fundisho kwa wengine
wenye nia ya kufanya mchezo mchafu kama huo.
Kwa kuwa Nida
wamefanya uandikishaji wa watumishi wa Serikali katika Jiji la Dar es
Salaam pekee, tunaamini kwamba kashfa hii si tu polisi na wanajeshi
pekee bali itagusa maeneo yote.
Mbaya zaidi kashfa za kutumia
vyeti bandia huenda vikaikumba sekta ya elimu ambayo kwa muda mrefu
imekuwa ikilalamikiwa kwamba elimu inayotelewa na baadhi ya walimu
haikidhi viwango halisi.
Matokeo yake, wanafunzi wengi wanaomaliza
elimu ya msingi nchini hawajui kusoma wala kuandika na kibaya zaidi
kuna wengine wenye udhaifu huo wanachaguliwa kuendelea na elimu ya
sekondari.
Sote tumeshuhudia askari wengi wakifanya kazi chini ya kiwango kumbe kuna tatizo la msingi nalo ni kutokuwa na elimu inayoendana na kazi wanayoifanya.
Lakini jambo muhimu la kujiuliza inakuwaje vyombo vya usalama ambavyo vina mkono mrefu vimeshindwa kufuatilia hawa watu kama kweli vyeti wanavyomiliki ni vyao? Je ndani ya vyombo vyetu vya usalama watumishi wote ni raia au kuna wageni? Yote haya ni majibu ambayo tume ya polisi inapaswa kuweka wazi kwa wananchi.
Tunadhani Serikali na vyombo vya dola vitachukulia sakata hili kwa umakini mkubwa ili wale wote wanaohusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ni maoni yetu kwamba wafanyakazi
wote ambao wamegushi vyetu vyao na kuajiriwa serikalini na katika sekata
binafsi waachie ngazi mara moja na hatua za kisheria zianze dhidi yao
kwa uvunjaji wa maadili ambao katu hauvumiliki.
0 comments:
Post a Comment