Mgombea urais kwa tiketi ya
chama cha kisoshalisti nchini Ufaransa Francois Hollande, ameshinda duru
ya kwanza ya uchaguzi nchini humo.
Kura nyingi zikiwa zimehesabiwa Bw Hollande tayari amepata asilimia 28 ya kura.
Haijawahi kutokea kuwa rais aliyemadarakani anashindwa kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.
Na matokeo haya yanampa mpinzani wa Rais
Sarkorzy, Francois Hollande nafasi nzuri sana katika duru ya pili ya
uchaguzi huo utakaofanyika baada ya wiki mbili.
Hata hivyo kilicho washangaza wengi baada ya
matokeo hayo kutangazwa ni idadi ya kura chama kinacho egemea upande wa
kulia kilipata.
Kwa makadirio tu, mtu mmoja kati ya wapiga kura
watano nchini Ufaransa alikipigia kura chama hicho, hii ikiwa idadi
kubwa zaidi ya kura chama hicho cha Front Nationale kilicho pata kwenye
uchaguzi wowote nchini humo.
Rais Sarkorzy anasema matokeo hayo yanaonyesha
hali ya wasi wasi raia wa nchi hiyo wanayo na ni kura ya maoni dhidi ya
utawala wake.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa mpinzani wake ajitokeze kwenye mdahalo kati yao kabla duru ya pili ya uchaguzi huo.
Lakini bila shaka kutokana na uchache wa kura
alizopata dhidi ya Rais Sarkorzy, kiongozi huyo wa chama cha
kisoshalisti, Francoise Hollande atakuwa makini sana asipoteze kura
muhimu.
Bw Hollande anasema wafaransa wanaimani na mradi
wake kwa nchi hiyo ambao umelenga kurejesha haki, usimamizi bora wa
uchumi wa nchi, ukuzaji wa nafasi za kazi, kulinda viwanda na kujiandaa
vyema kwa siku za usoni.
0 comments:
Post a Comment